Kijana mdogo wa miaka 21, raia wa Spain, Cesc Fabregas, anaechezea kama kiungo, leo ametangazwa kuwa ndie Nahodha mpya wa Klabu ya Arsenal kuchukua nafasi ya William Gallas alievuliwa cheo hicho majuzi baada ya kubatuka hadharani kuhusu mpasuko ndani ya klabu.
Kufuatia kitendo hicho, Gallas alitemwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichocheza LIGI KUU Jumamosi huko Manchester na Manchester City mechi ambayo Arsenal, ikiongozwa na Nahodha wa muda, Kipa Manuel Almunia, ilichabangwa mabao 3-0.
Uteuzi wa Fabregas umethibitishwa na Meneja Arsene Wenger alietamka: 'Fabregas ndie Nahodha wa kudumu. Sina haja ya kueleza kwa nini!'
Akaongeza: 'Gallas atacheza mechi ya kesho ila Kepteni ni Fabregas. Nimetoa uamuzi huu.'
Alipobanwa na kuhojiwa kama alifanya makosa kwa kumteua Gallas kama Nahodha, Wenger alisema: 'Hapana, sijutii kumfanya yeye Kepteni.'
No comments:
Post a Comment