Monday 24 November 2008

RONALDO APAA KWENDA EL MADRIGAL!

Mchezaji Bora Uingereza, Ulaya na kwa Wachezaji wa Kulipwa, Cristiano Ronaldo, amepaa pamoja na kikosi cha Manchester United kwenda Madrid, Spain kupambana na Villareal kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE uwanjani El Madrigal.

Ronaldo aliumizwa Jumamosi Man U ilipocheza na Aston Villa kwenye mechi ya LIGI KUU ambayo iliisha suluhu ya 0-0.

Katika mechi yote hiyo Ronaldo alionekana anawindwa na Aston Villa waliokuwa wakitumia miguvu, rafu na kila staili ya mchezo wa raga ili kumsimamisha.

Ilibidi Ronaldo apumzishwe kipindi cha pili cha mechi hiyo na baadae Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson aligusa kwamba huenda Ronaldo asiwemo kwenye kikosi kitakachoenda Spain.

Wachezaji ambao hawamo kwenye kikosi kilichosafiri ni Kipa Edwin Van der Sar [ anaepumzishwa], Dimitar Berbatov, Wes Brown, Gary Neville, chipukizi Danny Welbeck, Paul Scholes na Owen Hargreaves [ambao wote ni majeruhi].

Man U na Villareal wote wana pointi 8 ingawa Man U inaongoza KUNDI hili kwa magoli.

Kila timu inahitaji pointi moja tu kuhakikisha iinaingia raundi inayofuata.

No comments:

Powered By Blogger