Monday 24 November 2008

MECHI ZA JANA LIGI KUU:

Tottenham 1 Blackburn 0

Jana Tottenham, ikicheza kwake White Hart Lane, ilijikwamua kutoka kwenye klabu tatu za chini katika msimamo wa ligi baada ya kuifunga Blackburn Rovers bao 1-0 katika mechi ambayo Beki wa pembeni kushoto Martin OLsson alitolewa nje kwenye dakika ya 39 baada ya kulambwa Kadi yake ya pili ya Njano na Refa Howard Webb.
Winga Aaron Lennon wa Tottenham ndie aliekuwa Mchezaji Bora wa mechi hii na alimtesa sana mkabaji wake Martin Olsson na alimudu kumpora mpira kwenye dakika ya 9 na kuingia nao ndani ya boksi kisha kupiga vii murua iliyounganishwa utamu na Mshambuliaji Mrusi Roman Pavlyuchenko na kutinga wavuni.
Winga Aaron Lennon aliendelea kumtesa Beki kutoka Sweden Martin Olsson na kumsababisha apewe Kadi ya Njano dakika ya 26 iliyofuatiwa na nyingine ya pili dakika ya 39 na hivyo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Tottenham: Gomes, Corluka, Woodgate, King, Assou-Ekotto, Bentley (O'Hara 86), Jenas, Huddlestone, Lennon, Pavlyuchenko (Campbell 74), Bent.
Akiba [Hawakucheza]: Cesar, Bale, Zokora, Gunter, Dawson.
Kadi: Bentley, Jenas.
Goli: Pavlyuchenko

Blackburn: Robinson, Ooijer, Samba, Nelsen, Olsson, Emerton (Derbyshire 71), Andrews, Mokoena, Pedersen (Treacy 81), McCarthy (Simpson 46), Roque Santa Cruz.
Akiba [hawakucheza]: Brown, Kerimoglu, Fowler, Roberts.
Kadi Nyekundu: Olsson
Kadi: Olsson, Ooijer, Andrews.
Watazamaji: 35,903
Refa: Howard Webb

Sunderland 0 West Ham 1

Goli lililofungwa na Valon Behrami [pichani wa kushoto] katika dakika ya 20 limewapa West Ham ushindi wao wa kwanza katika mechi 8 zilizopita.
Bao hio lilifungwa baada ya kumbabatiza Mchezaji wa Sunderland Kenwyne Jones na kumchuuza Kipa Marton Fulop.
Sunderland , wakiwa nyumbani Stadium of Light, walicheza chini ya kiwango na kukosa nafasi kadhaa za dhahiri kupitia kwa Mshambuliaji wao wa Kifaransa Djibril Cisse.
Na ili kudhihirisha haikuwa siku yao hata Refa Mike Dean aliwanyima penalti za wazi pale Washambuliaji wao Djibril Cisse na Kenwyne Jones walipoangushwa ndani ya boksi.
Kipigo hiki ni cha 4 kwa timu ya Sunderland inayoongozwa na Meneja Roy Keane wakiwa nyumbani kwao msimu huu na cha 3 mfululizo.

Sunderland: Fulop, Bardsley, Nosworthy, Ferdinand, Collins, Malbranque (Edwards 66), Whitehead, Reid (Murphy 66), Richardson, Jones (Diouf 81), Cisse.
Akiba [hawakucheza]: Colgan, Tainio, Colback, Henderson.
Kadi: Reid, Bardsley.

West Ham: Green, Neill, Collins, Upson, Ilunga, Faubert (Boa Morte 76), Parker, Bowyer (Mullins 61), Behrami, Bellamy (Di Michele 87), Cole.
Akiba [hawakucheza]: Lastuvka, Davenport, Collison, Sears.
Kadi: Bowyer.
Goli: Behrami 20.
Watazamaji: 35,222.
Refa: Mike Dean

No comments:

Powered By Blogger