FA Cup: Arsenal nje!!!
• Stoke City 3 Arsenal 1
Sol Campbell leo ameanza kibarua chake Arsenal kwa kipigo kwenye Uwanja wa Britannia cha 3-1 na Stoke City kwenye mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la FA na hivyo kubwagwa nje ya Mashindano hayo.
Arsenal wakichezesha Kikosi cha mchanganyiko cha Maveterani kama kina Campbell na Silvestre na Chipukizi kina Eastmond, Coqquelin na Vela walijikuta wako nyuma baada ya dakika moja tu mechi kuanza baada ya silaha yao kubwa ya Stoke City ya mipira ya kurushwa ya Rory Delap kutumika na mpira huo wa kurusha kumkuta Straika Ricardo Fuller ndani ya boksi aliemaliza kwa kichwa.
Arsenal walisawazisha dakika ya 44 baada ya frikiki ya Fabregas kupasiwa Denilson aliefumua shuti lililobabatiza Wachezaji wawili wa Stoke na kumhadaa Kipa Sorensen na kutikisa nyavu.
Alikuwa Fuller tena aliepachika bao la pili dakika ya 77 baada ya Sidibe kumfunga tela Denilson winga ya kulia na kutia krosi iliyopigwa kichwa na Fuller.
Dean Whitehead akapigilia nsumari wa mwisho dakika ya 86 kwa bao tamu na kuifanya Arsenal kujumuika na Manchester United na Liverpool kuwa Watazamaji maarufu wa FA Cup.
Vikosi vilivyoanza:
Stoke: Sorensen, Huth, Shawcross, Higginbotham, Collins, Delap, Whitehead, Whelan, Etherington, Sidibe, Fuller.
Akiba: Simonsen, Lawrence, Beattie, Pugh, Diao, Sanli, Wilkinson.
Arsenal: Fabianski, Coquelin, Campbell, Silvestre, Traore, Eastmond, Denilson, Fabregas, Walcott, Emmanuel-Thomas, Vela.
Akiba: Mannone, Rosicky, Eduardo, Ramsey, Arshavin, Bartley, Frimpong.
Refa: Martin Atkinson
FA Cup: Dro ya Raundi ya 5 kufanyika leo usiku!!
Mabingwa Watetezi Chelsea pamoja na Timu nyingine 11 za Ligi Kuu wanasubiri kujua watapangiwa kucheza na nani katika mechi za Raundi ya 5 ya Kombe la FA zitakazochezwa Februari 12 na 13.
Dro ya mechi hizo inafanyika leo Jumapili Januari 24 saa 3 usiku saa za bongo.
Timu zitakazopigiwa kura ni:
1 Southampton
2 Reading
3 Derby County
4 Cardiff City
5 Stoke City
6 Notts County au Wigan Athletic [mechi inarudiwa]
7 Scunthorpe United au Manchester City [mechi inachezwa saa hizi]
8 West Bromwich Albion
9 Birmingham City
10 Fulham
11 Bolton Wanderers
12 Portsmouth
13 Chelsea
14 Aston Villa
15 Wolverhampton Wanderers au Crystal Palace [mechi inarudiwa]
16 Tottenham Hotspur au Leeds United [mechi inarudiwa]
No comments:
Post a Comment