Monday 8 February 2010

Ballack: ‘Bingwa ni sisi Chelsea au Man United, Arsenal nje!!’
• Ambatukia Wenger aache visingizio!
Kiungo wa Chelsea Michael Ballack ametamka kuwa Ubingwa wa England sasa unagombewa na Timu mbili tu, Chelsea na Manchester United, na amemtaka Arsene Wenger aache kutoa visingizio kwa Arsenal kutokuwa na uwezo wa kuwafunga wapinzani wao.
------------------------------------------------------------------------------
MSIMAMO KILELENI MWA LIGI:
 [TIMU ZIMECHEZA MECHI 25 ISIPOKUWA INAPOTAJWA]
1 Chelsea pointi 58
2 Man Utd pointi 56
3 Arsenal pointi 49
4 Liverpool pointi 44
5 Tottenham pointi 43
6 Manchester City pointi 41 [mechi 23]
7 Aston Villa pointi 41 [mechi 24]
------------------------------------------------------------------------------ 
Ballack amesema Arsenal ishajulikana na inatambulika uchezaji wake na wapinzani wake na kamwe hawawezi kuchukua Kikombe chochote kwa sasa [Kombe lao la mwisho kuchukua ni FA Cup mwaka 2005] mpaka hapo Wenger atakapoibadilisha na kuifanya iweze kutumia mbinu tofauti uwanjani.
Arsenal wamevikwaa vipigo viwili mfululizo na wapinzani wao wakubwa cha kwanza kikiwa Jumapili iliyopitwa walipochapwa 3-1 na Manchester United na jana kufungwa 2-0 na Chelsea na sasa wako nafasi ya 3 wakiwa pointi 9 nyuma ya Chelsea na pointi 7 nyuma ya Manchester United.
Akimjibu Wenger aliedai Timu nzuri ndio iliyofungwa, Ballack alisema: “Nadhani siku zote anasema hivyo wakifungwa. Wakifungwa siku zote hutoa visingizio. Soka si kumiliki mpira tu. Soka ni kushinda na siku zote tukicheza nao sisi tunacheza kushinda si kumiliki mpira.”
Wadau wengi ambao ni wataalam wa kandanda wanadai Arsenal haina uwezo wa kubadili mbinu ikiwa uwanjani kuibadili soka yao ya kutandaza pasi na kushambulia kwa nguvu ili kufunga mabao na pia haina ubavu wa kuhimili mikikimikiki ya Timu zinazotumia ubavu.
WAFUNGAJI BORA LIGI KUU:
-Rooney [Man United] mabao 21
-Drogba [Chelsea] mabao 17
-Defoe [Tottenaham] 15
-Bent [Sunderland] 14
-Tevez [Man City] 12
-Torres [Liverpool] 12
-Fabregas [Arsenal] 11
-Saha [Everton] 11
-Agbonlahor [Aston Villa] 10
-Lampard [Chelsea] 10
-Kuyt [Liverpool] 9
-Adebayor [Man City] 8
-Anelka [Chelsea] 8
-Berbatov [Man United] 8
-Arshavin [Arsenal] 7

No comments:

Powered By Blogger