Monday, 8 February 2010

Chelsea kicheko tu!!!
• Wamsapoti Nahodha John Terry
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti na Shujaa wao Mfungaji wa bao zao za jana Ddier Drogba wamejipongeza kwa ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Arsenal uliowafanya watwae tena uongozi wa Ligi Kuu kwa kummwagia sifa Nahodha wao John Terry aliendamwa na kashfa ya kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge na kumfanya atimuliwe Unahodha wa England.
Mara baada ya mechi ya jana, Drogba alisema: “Ni wiki ngumu kwetu! Tulimsapoti sana Nahodha Terry!! Ni vyema alicheza na tumeshinda kwani hilo linamtuliza.”
Nae Ancelotti alisema: “Ni Kepteni bora kwetu. Uamuzi wa England si wangu! Kwetu ni mtu safi! Alicheza mechi hii vizuri sana!”
Ancelotti alikataa kuifuta Arsenal kwenye mbio za Ubingwa na amesema Arsenal ni Timu nzuri ila itategemea Chelsea na Manchester United wana mafanikio gani katika mechi zao.
Wenger akiri Ubingwa kwao ni nje ya uwezo!!!
Kufuatia kipigo cha Stamford Bridge hapo jana mikononi mwa Chelsea cha bao 2-0 za Didier Drogba, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amekiri Ubingwa wa Ligi Kuu uko nje ya uwezo wao ingawa amesema hawajakata tamaa.
Wenger ametamka: “Sasa tupo nje ya kinyang’anyiro lakini hatujakata tamaa! Tutapigana mpaka siku ya mwisho! Naamini kila mtu atapoteza pointi. Lazima tushinde Jumatano na Liverpool halafu tutajua tumesimama wapi!”
Kipigo cha jana cha Chelsea kimeifanya Timu ya Wenger iwe kwenye wakati mbaya kwa wiki moja iliyopita kwani Jumapili iliyopita walibamizwa 3-1 na Manchester United nyumbani kwao Emirates.
Wenger amechambua mechi ya jana kwa kusema: “Tulimiliki mpira zaidi ya asilimia 70. Tulikuwa tunashambulia lakini kwenye mechi kubwa ukiwa 2-0 nyuma ni mambo magumu sana! Chelsea walijihami vizuri”
Hata hivyo aliiponda Chelsea kwa kudai kuwa hawakuwa wabunifu na waliharibu soka.
Wenger alisema amefurahishwa na uchezaji wa Timu yake ukilinganisha na mechi ya Manchester United waliyozidiwa kila kitu.
Mchezaji alia na Refa!!!
Straika wa Bolton Kevin Davies amemponda Refa Mark Clattenburg baada ya kulikataa goli lake safi ambalo lingeipata ushindi Timu yake ilipocheza na Fulham katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Reebok Stadium na kwisha 0-0 hapo Jumamosi.
Davies amedai: “Kila mara akituchezesha, Clattenburg anatuonea! Nilipojua Refa ni nani nilijua hatupati kitu! Siku zote naamini Refa huyo ana chuki binafsi na sisi au mimi!!”
KWINGINEKO ULAYA: MATOKEO 
SERIE A:
Jumapili, Februari 7
Atalanta 1 v Bari 0
Inter Milan 3 v Cagliari 0
Lazio 0 v Catania 1
Bologna 0 v AC Milan 0
Udinese 3 v Napoli 1
Siena 1 v Sampdoria 2
Genoa 1 v Chievo Verona 2
LA LIGA:
Jumapili, Februari 7
Osasuna 1 v Tenerife 0
Racing Santander 1 v Atletico Madrid 1
Athletic Bilbao 3 v Xerez 2
BUNDESLIGA:
Jumapili, Februari 7
Mainz 05 1 v Borussia Moenchengladbach 1
Borussia Dortmund 2 v Eintracht Frankfurt 3

No comments:

Powered By Blogger