Saturday 13 February 2010

FA Cup: Reading v WBA sare, Birmingham washinda dakika za mwisho!
Birmingham wametinga Robo Fainali ya Kombe la FA kwa goli la ushindi lililofungwa na Liam Ridgewell dakika ya 91 na kuwafanya Birmingham waishinde Derby bao 2-1.
Derby ndio waliopata bao la kwanza dakika ya 55 kupitia McEveley na Birmingham wakarudisha dakika ya 73 mfungaji akiwa Dann.
Na West Bromwich Albion walikuwa nyuma kwa bao 2-1 dhidi ya Reading hadi dakika ya 87 ndipo Mattock akasawazisha na Timu hizi zitarudiana huko Hawthorns, Uwanja wa West Bromwich, hapo Februari 24.
CAF CHAMPIONS LEAGUE: Yanga yadundwa Bongo!!
Leo, katika mechi ya Raundi ya awali kugombea Klabu Bingwa Afrika, Mabingwa wa Bongo, Yanga, wamefungwa 3-2 wakiwa nyumbani na Mabingwa wa Congo DR [ile ya Kabila] FC Saint Eloi Lupopo.
Huko Kenya katika Kombe hilohilo la Klabu Bingwa Afrika, Sofapaka ya Kenya ilitoka sare 0-0 na El Ismaily ya Misri
Capello aweweseka kuhusu Rooney!
Ambembeleza Fergie awe anampumzisha!
Fabio Capello, Meneja wa England, amemwomba Sir Alex Ferguson asimchezeshe Wayne Rooney kila mechi ili apumzike na ikifika Juni kwenye Fainali za Kombe la Dunia awe bado yuko freshi.
Ombi la Capello huenda lisisikilizwe kwa vile Rooney pia ni muhimu sana kwa Manchester United wanaowania kuutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya 4 mfululizo, wako Fainali ya Carling watakayocheza na Aston Villa hapo Februari 28 na pia wako Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na wanacheza mechi mbili na AC Milan katika mtoano huo.
Rooney ndie anaongoza na tegemezi kubwa kwa magoli Manchester United.
Wadau wanahisi ombi la Capello limekuja wakati England ina wasiwasi wa kumpoteza Beki wa kushoto, Ashley Cole, ambae amevunjika enka na imekadiriwa atarudi uwanjani mwezi Mei na kuna hisia muda huo ni mfupi mno kwa Cole kujijenga kuwa fiti tena kwa Fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni.

No comments:

Powered By Blogger