Sunday, 7 February 2010

Tottenham 0 Aston Villa 0
Tottenham na Aston Villa jana walivimbiana Uwanja wa White Hart Lane na hakuna mbabe aliepatikana na ngoma kuisha 0-0 katika mechi ya Ligi Kuu.
Makipa wa pande zote, Brad Friedel wa Aston Villa na Heurelho Gomes, walistahili pongezi kwa kuziokoa Timu zao.
Kwa Timu hizi mbili ushindi ulikuwa muhimu ili kuipiku Liverpool toka nafasi ya 4 waliyoichukua katika mechi iliyochezwa kabla ya hii walipowafunga Everton 1-0 na kufikisha pointi 44 kwa mechi 25.
Kwa sare hiyo Tottenham wamebaki nyuma ya Liverpool na wana pointi 43 kwa mechi 25 wakifuata Man City wenye pointi 41 kwa mechi 23 na Aston Villa pointi 41 kwa mechi 24.
Baada ya Mechi, Meneja wa Tottenham Harry Redknapp alisema: “Kila tukitaka kufunga mpira unambabatiza mtu au unazuiawa! Itakuwa kazi kubwa kuipata nafasi ya 4 au hata ya tatu! Liverpool wanaenda vizuri, Man City na Villa wapo pia!”
Na Meneja wa Aston Villa Martin O’Neill akasema: “Mabeki wetu walikuwa makini. Tottenham ni timu ngumu!”
KWINGINEKO ULAYA: MATOKEO YA WIKIENDI NA RATIBA YA LEO
SERIE A:
Jumamosi, Februari 6
Livorno 0 v Juventus 0
Palermo 2 v Parma 1
Jumapili, Februari 7
Atalanta v Bari
Inter Milan v Cagliari
Lazio v Catania
Bologna v AC Milan
LA LIGA:
Jumamosi, Februari 6
Valencia 2 v Valladoid 0
Barcelona 2 v Getafe 1
Real Madrid 3 v Espanyol 0
Jumapili, Februari 7
Osasuna v Tenerife
Racing Santander v Atletico Madrid
Athletic Bilbao v Xerez
BUNDESLIGA
Ijumaa, Februari 5
Werder Bremen 2 v Hertha Berlin 1
Jumamosi, Februari 6
Freiburg 0 v Schalke 0
Wolfsburg 1 v Bayern Munich 3
1899 Hoffenheim 2 v Hannover 1
Bochum 1 v Bayer Leverkusen 1
Cologne 3 v Hamburg 3
Nurnberg 1 v Stuttgart 2
Jumapili, Februari 7
Mainz 05 v Borussia Moenchengladbach
Borussia Dortmund v Eintracht Frankfurt

No comments:

Powered By Blogger