Wednesday 10 February 2010

MECHI ZA JANA LIGI KUU:
Portsmouth 1 Sunderland 1
Portsmouth walinusurika kufungwa pale Aruna Dindane alipowasawazishia dakika ya 96
na kuifanya mechi na Sunderland imalizike 1-1.
Sunderland walipata bao lao kupitia Darren Bent kwa penalti baada ya Beki wa Portsmouth Ricardo Rocha kumuangusha Bent ndani ya boksi na Refa akatoa penalti na kumpa Kadi Nyekundu Rocha.
Man City 2 Bolton 0
Mabao ya Tevez na Adebayor yamewawezesha Manchester City kutinga nafasi ya 5 kwenye Ligi baada ya kuifunga Bolton 2-0 hapo jana.
Bao la Tevez lilifungwa kwa penalti baada ya Paul Robinson wa Bolton kumuangusha Adam Johnson ndani ya boksi.
Fulham 3 Burnley 0
Fulham walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Burnley kwa mabao ya Danny Murphy, Elm na Bobby Zamora.
Mpaka mapumziko Fulham walikuwa mbele kwa mabao mawili ambayo wengi wanaamini hayakustahili kwa vile tote yalifungwa wakati kulikuwa na ofsaidi za wazi.
Baada ya mechi Meneja wa Burnley, Brian Laws, alilalamika: “Tuliona wazi bao zao mbili ni ofsaidi! Ingawa hatukucheza vizuri lakini siku zote unataka haki kwa Refa!”
Wigan 1 Stoke City 1
Tuncay aliisawazishia Stoke na kuifanya Timu yake iwe haijafungwa mwaka huu na kuwanyima ushindi Wigan waliopataka bao lao kupitia Paul Scharner.
Meneja wa Stoke Tony Pulis alieleza: “Wigan walikuwa bora kipindi cha kwanza lakini sie tulibadilika baadae!”
Nae Roberto Martinez wa Wigan alisema: “Inavunja moyo ukiongoza halafu ukaukosa ushindi lakini angalau tumepata pointi moja!”
Ronaldinho nje Brazil!!
Ronaldinho,miaka 29, ambae sasa ameanza kung’ara tena na Klabu yake AC Milan hayumo kwenye Kikosi cha Brazil kilichoteuliwa kucheza mechi ya kirafiki hapo Machi 2 na Ireland kwenye Uwanja wa Emirates, nyumbani kwa Arsenal, na hivyo kuleta hisia huenda asiwemo kwenye Timu ya Brazil itakayocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni.
Ronaldinho hajaichezea Brazil tangu mwanzoni mwa 2009 na licha ya kelele za Mashabiki huko Brazil na hata wito kutoka Mchawi Pele wa kutaka Ronaldinho aingizwe Kikosini, Kocha wa Brazil Dunga amemuacha Nyota huyo.
Kikosi kamili cha Brazil na Klabu wanazotoka ni:
MAKIPA: Julio Cesar (Inter Milan), Doni (Roma).
WALINZI: Maicon (Inter Milan), Daniel Alves (Barcelona), Gilberto (Cruzeiro), Michel Bastos (Lyon), Juan (Roma), Lucio (Inter Milan), Luisao (Benfica), Thiago Silva (AC Milan).
VIUNGO: Gilberto Silva (Panathinaikos), Josue (Wolfsburg), Felipe Melo (Juventus), Lucas (Liverpool), Kaka (Real Madrid), Ramires (Benfica), Elano (Galatasaray), Julio Baptista (Roma), Kleberson (Flamengo).
MAFOWADI: Robinho (Santos), Adriano (Flamengo), Nilmar (Villarreal), Luis Fabiano (Seville).

No comments:

Powered By Blogger