Sunday 7 February 2010

DROO YA EURO 2012: Tayari, Makundi yapangwa!!!
England imepangwa Kundi moja na Wapwa zao Wales katika Kundi G kuwania kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazofanyika katika Nchi mbili, Poland na Ukraine, kwa pamoja.
Nchi nyingine kwenye Kundi la England ni Switzerland, Bulgaria na Montenegro.
Makundi yapo 9 na Makundi 6 yana Nchi 6 na matatu yana Nchi 5.
Fainali hizo za EURO 2012 zitachezwa kuanzia Juni 8, 2012 hadi Julai 1, 2012 na kuna nafasi 14 zinazogombewa na hayo Makundi 9 kujumuika na Wenyeji Poland na Ukraine kufanya jumla ya Timu 16 katika hizo Fainali.
Mechi za Makundi zitachezwa kuanzia Septemba 2010 na kumalizika Oktoba 2011.
Washindi 9 wa Makundi pamoja na Timu moja iliyo nafasi ya pili bora kuliko zote zilizoshika nafasi hiyo ndizo zitaingia Fainali moja kwa moja.
Timu nyingine 8 zilizoshika nafasi ya pili zitapangiwa mechi maalum za mtoano ili kupata Timu 4 zitakazoenda Fainali.
MAKUNDI NI:
KUNDI A: Azerbaijan, Kazakhstan, Belgium, Austria, Turkey, Germany
KUNDI B: Andorra, Armenia, Macedonia, Republic of Ireland, Slovakia, Russia
KUNDI C: Faroe Islands, Estonia, Slovenia, NORTHERN IRELAND , Serbia, Italy
KUNDI D: Luxembourg, Albania, Belarus, Bosnia, Romania, France
KUNDI E: San Marino, Moldova, Hungary, Finland, Sweden, Netherlands
KUNDI F: Malta, Georgia, Latvia, Israel, Greece, Croatia
KUNDI G: Montenegro, WALES , Bulgaria, Switzerland, ENGLAND
KUNDI H: Iceland, Cyprus, Norway, Denmark, Portugal
KUNDI I: Liechtenstein, Lithuania, SCOTLAND , Czech Republic, Spain

No comments:

Powered By Blogger