Friday 12 February 2010

NI MAJERUHI TU:
• Ashley Cloe nje miezi mitatu, Kombe la Dunia hatihati kwake!
• Giggs auti mwezi!
• Arsenal wapo kibao!
Mechi za Ligi Kuu za katikati ya wiki zimezua balaa kwa baadhi ya Klabu na zitapoteza Wachezaji wao muhimu katika kipindi hiki muhimu tukielekea ukingoni mwa Ligi.
Ashley Cole wa Chelsea alitolewa kipindi cha pili cha mechi ya Jumatano ambayo Chelsea walifungwa 2-1 na Everton na jana imethibitika kuwa amevunjika enka na atakuwa nje kwa miezi mitatu.
Hilo ni pigo kubwa si tu kwa Chelsea bali pia kwa England kwani Cole ni Beki wa kushoto wa kutumainiwa na kuumia huku kuna maana atarudi uwanjani mwezi Mei wakati Kombe la Dunia England inacheza mechi ya kwanza Juni 12 na USA.
Klabuni kwake, nafasi ya Cole inaweza kuzibwa na Yuri Zhirkov na hata Beki wa kulia Paulo Ferrera.
Kwa England, nafasi yake huenda ikazibwa na Wayne Bridge Mchezaji alievutwa kwenye kashfa ya John Terry kwani gekfrendi wake wa zamani ambae amezaa nae mtoto anadaiwa kutembea na John Terry, ambae ni mwanandoa, na hilo limesababisha Terry atimuliwe Unahodha wa England.
Kashfa hiyo inadaiwa kutokea wakati wote Bridge na Terry ni Wachezaji wa Chelsea.
Kwa sasa Bridge yupo Manchester City.
Huko Manchester United kuna pigo la kumkosa Mkongwe Ryan Giggs ambae alivunjika mkono kwenye droo ya 1-1 ya Ligi Kuu na Aston Villa baada ya kugongana na Steve Sidwell wa Villa na ikabidi abadilishwe.
Man United imethibitisha Giggs atakosekana kwenye mechi ijayo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Milan, Italia watakapocheza na AC Milan Jumanne Februari 16.
Vilevile, atazikosa mechi za Ligi Kuu dhidi ya Everton, Wolves na West Ham na pia Fainali Kombe la Carling hapo Februari 28 Man U watakapovaana na Aston Villa Wembley Stadium.
Man United imesema mechi ya kwanza ambayo Giggs ataweza kucheza ni ile ya marudiano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na AC Milan hapo Machi 10 uwanjani Old Trafford.
Nao Arsenal, ambao hawana mechi wikiendi hii kwa vile wameshatolewa Kombe la FA, mechi yao inayofuata ni Jumatano huko Ureno watakapocheza na FC Porto kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, wanakabiliwa na kuumia kwa Andrey Arshavin na Alex Song kwenye mechi ya Ligi Jumatano na Liverpool ambayo walishinda 1-0.
Meneka wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema inabidi uchunguzi ufanywe kwa Wachezaji hao.
Hata hivyo, Fowadi wao wa Croatia mwenye asili ya Brazil Eduardo amepona na huenda akachezeshwa mechi hiyo na FC Porto.

No comments:

Powered By Blogger