Saturday 13 February 2010

FA Cup: Chelsea, Portsmouth ndani ya Robo Fainali!!
Mabingwa Watetezi wa FA Cup, Chelsea, na Klabu iliyo kwenye msukosuko mkubwa wa kifedha, Portsmouth, leo wametinga Robo Fainali ya Kombe la FA baada ya kuwabwaga wapinzani wao kwa bao 4-1 kila mmoja.
Chelsea wakicheza kwao Stamford Bridge waliitwanga Cardiff City 4-1 kwa bao za Drogba, Ballack, Sturridge na Kalou.
Bao la Cardiff lilifungwa na Michael Chopra.
Portsmouth wakiwa wageni wa Southampton walishinda bao 4-1 huku bao zote za mechi hiyo zikiingia kipindi cha pili.
Portsmouth ndio waliotangulia kwa bao la Owusu-Abeyie lakini Southampton wakasawazisha kupitia Rickie Lambert.
Portsmouth wakaongeza bao 3 zilizofungwa na Arune Dindane, Nadir Belhadj na Jamie O’Hara.
Leo bado kuna mechi nyingine tatu za FA mbili zitaanza baada ya muda si mrefu, Derby v Birmingham na Reading v WBA, na ya tatu, Man City v Stoke, itaanza saa 2 na robo, saa za bongo.

No comments:

Powered By Blogger