Sunday 7 February 2010

Kipigo kingine kwa Arsenal!!
• Drogba awapiga viwili!!!
Goli mbili za Didier Drogba, dakika ya 7 na 23, zimewaua tena Arsenal kwenye Ligi Kuu na kuwapaisha tena Chelsea kuipiku Manchester United na kuchukua uongozi wa Ligi sasa wakiwa na pointi 58 na Man United wakiwa nafasi ya pili na wana pointi 56.
Arsenal wamebaki nafasi ya 3 wakiwa na pointi 49.
Katika mechi hii Chelsea walitumia mbinu ya kudifendi na kuwaacha Arsenal washambulie na kisha wao kutegemea kuunasa mpira na kufanya shambulizi la nguvu na haraka.
Mbinu hiyo ilifanikiwa mno na ndio iliozaa bao la pili baada ya kaunta ataki ya Chelsea kufanikiwa na Drogba kufunga bao hilo la pili.
Bao la kwanza la Chelsea lilitokana na kona ambayo Arsenal walishindwa kujipanga vizuri na kichwa cha Nahodha wao Terry kumkuta Drogba akiwa pembeni na kupachika kilaini.
Juu ya Chelsea kudifendi vizuri Arsenal nao inabidi wajilaumu wenyewe kwani walimiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini zile mbwembwe za ‘soka tamu’ ndio tatizo lao kubwa huku wakitaka ‘watembee na mpira’ mpaka wavuni.
Sasa, pengine, karata ya mwisho ya Arsenal ipo Jumatano watakapocheza na Liverpool na wakifungwa tu hata hiyo nafasi yao ya 3 iko hatarini kwani Liverpool akishinda mechi hiyo atakuwa na pointi 47 zikiwa pointi 2 tu nyuma ya Arsenal.
Vikosi vilivyyoanza:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Carvalho, Terry, Cole, Mikel, Lmpard, Malouda, Ballack, Drogba, Anelka
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Walcott, Fabregas, Song, Diaby, Arshavin, Nasri
Refa: Mike Dean
Birmingham 2 Wolves 1
Katika mechi ya Ligi kuu iliyoitangulia ile Bigi Mechi ya Chelsea v Arsenal Wolves walitangulia kufunga bao na kuongoza hadi mapumziko lakini Mkongwe Kevin Phillips, miaka 36, akitokea benchi aliifungia Birmingham bao mbili dakika za mwishoni na kuwapa ushindi wa 2-1.

No comments:

Powered By Blogger