Thursday 11 February 2010

Terry apewa mapumziko
Chelsea imethibitisha kuwa Nahodha wao John Tery hataonekana kwenye mechi ya FA Cup watakapocheza na Cardiff siku ya Jumamosi kwa sababu amepewa mapumziko mafupi na atarudi Uwanjani Februari 20 Chelsea watakapocheza na Wolves kwenye Ligi Kuu.
Terry, ambae anakabiliwa na kashfa nzito ya kutembea na gelfrendi wa Wayne Bridge aliekuwa Mchezaji mwenzake Chelsea na hata kusababisha kutimuliwa Unahodha England, jana alicheza katika kipigo cha Chelsea cha 2-1 walichokipata toka kwa Everton na goli zote zinadaiwa ni makosa ya Terry.
Inaaminika Terry atafunga safari kwenda Dubai aliko Mkewe ili kutafuta amani kufuatia kashfa yake. 
Ferguson: Nyekundu kwa Nani sawa!
Wengi waliamini Kadi Nyekundu aliyopewa Winga Nani kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo jana kati ya Aston Villa na Manchester United ilikuwa ni makosa kwa vile alionekana wazi kuucheza mpira, Meneja wake, Sir Alex Ferguson, amekiri Refa Peter Walton alikuwa sahihi kumpa Kadi Nyekundu Nani.
Kutolewa huko kwa Nani kunamaanisha kafungiwa mechi 3 na hivyo hawezi kucheza Fainali ya Kombe la Carling dhidi ya Aston Villa hapo Februari 28 na pia atazikosa mechi za Ligi kabla ya hapo za Everton na West Ham.
Wakati huo huo, Ferguson amesema Veterani Ryan Giggs alipelekwa Hospitali kupiga eksirei mkono wake baada ya kuumizwa na Steve Sidwell hapo jana kwenye mechi ya Ligi na Aston Villa na haijajulikana ameumia kiasi gani na huenda akaikosa mechi ijayo na AC Milan.
Wikiendi hii Manchester United haina mechi kwa vile kuna mechi za FA Cup tu na wao washatolewa.
Mechi yao inayofuata ni Jumanne Februari 16 huko Milan, Italia watakapocheza na AC Milan kwenye Raundi ya Mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

No comments:

Powered By Blogger