Saturday 13 February 2010

Kadi ya Boateng yafutwa!!
Kiungo wa Hull City, Geoge Boateng, ameondolewa Kadi Nyekundu na hivyo kukwepa kufungiwa mechi 3 baada ya kubandikwa Kadi hiyo na Refa Lee Probert katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumatano huko Ewood Park na wenyeji Blackburn Rovers waliifunga Hull bao 1-0.
Kamisheni Huru ya Nidhamu imeifuta Kadi hiyo ya Boateng aliyopewa baada ya kuridhishwa waligongana vichwa kwa bahati mbaya na Mchezaji wa Blackburn Morten Gamst Pedersen.
Saha anaisapoti, ataka Man United iwe Bingwa!!
Baada ya kuiua Chelsea Jumatano kwa kuiwekea Everton bao 2 toka mguuni kwake na kuipa Everton ushindi wa bao 2-1 na hivyo kuisaidia Klabu yake ya zamani Manchester United kuisogelea Chelsea kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Straika Luis Saha amedai Manchester United ndio watakaotwaa Ubingwa msimu huu.
Kabla ya kujiunga na Everton, Saha alikuwa na Manchester United kwa miaka minne lakini muda mwingi alikuwa akijiuguza kwa kuumia mara kwa mara.
Saha ametamka: “Ningefurahi mno kama ningeweza kusema Everton ndie Bingwa lakini hilo haliwezi kutokea! Itakuwa mshikemshike kati ya Chelsea na Man United! Ingawa Chelsea wana nguvu, Ubingwa ni wa Man United kwa vile ni Timu nzuri zaidi! Wakishinda ntafurahi sana!”
Saha ameongeza kwa kusema bado ana mawasiliano ya karibu na Wachezaji wa Manchester United hasa Evra, Rooney na Hargreaves na walimpongeza kwa ushindi wa Jumatano.
Jumamosi ijayo Everton inaikaribisha Manchester United Goodison Park kwenye mechi ya Ligi Kuu.

No comments:

Powered By Blogger