Thursday 11 February 2010

LIGI KUU: MATOKEO Mechi za Jumatano 
Chelsea yafa, Arsenal kidedea, Man United ngoma ngumu!!
MATOKEO KAMILI:
Blackburn 1 Hull City 0
Everton 2 Chelsea 1
Arsenal 1 Liverpool 0
Aston Villa 1 Manchester United 1
West Ham 2 Birmingham 0
Wolves 1 Tottenham 0
Arsenal 1 Liverpool 0
Bao la Abou Diaby limewapa ushindi Arsenal dhidi ya Liverpool na kuwapa faraja kubwa wapenzi wa Arsenal baada ya kupata vipigo viwili mfululizo.
Arsenal wanaendelea kushikilia nafasi ya 3 kwenye Ligi na wako pointi 5 nyuma ya Man United ambao ni wa pili huku Chelsea wakiwa juu pointi moja mbele ya Man United.
Vikosi:
Arsenal: Almunia, Eboue, Gallas, Vermaelen, Clichy, Fabregas, Song, Diaby, Nasri, Bendtner, Arshavin.
Akiba: Fabianski, Sagna, Rosicky, Walcott, Denilson, Traore, Campbell.
Liverpool: Reina, Carragher, Skrtel, Agger, Insua, Lucas, Mascherano, Kuyt, Gerrard, Maxi, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Riera, Aurelio, Babel, Spearing, Degen, Kelly.
Refa: Howard Webb
Everton 2 Chelsea 1
Mabao mawili ya Luis Saha yamewaua Chelsea na kuwapa ushindi Everton wakiwa kwao Goodison Park lakini Chelsea bado wako juu Ligi Kuu kwa pointi 1 baada ya Man United kutoka sare na Aston Villa.
Chelsea ndio waliopata bao la kuongoza kupitia Malouda dakika ya 17 lakini Everton wakarudisha kupitia Saha.
Katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza Everton walipewa penalti baada ya Carvalho kumwangusha Donovan ndani ya boksi na Saha akakosa kufunga.
Kipindi cha pili, Saha akafunga bao na kuipa ushindi Everton.
Vikosi:
Everton: Howard, Neville, Heitinga, Distin, Baines, Donovan, Arteta, Osman, Bilyaletdinov, Cahill, Saha.
Akiba: Nash, Vaughan, Gosling, Yakubu, Senderos, Rodwell, Coleman.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Carvalho, Terry, Ashley Cole, Lampard, Mikel, Zhirkov, Anelka, Drogba, Malouda.
Akiba: Hilario, Ballack, Paulo Ferreira, Kalou, Sturridge, Matic, Bruma.
Refa: Alan Wiley
Aston Villa 1 Manchester United 1
Manchester United wakicheza mtu 10 kwa muda mrefu baada ya Mchezaji wao Nani kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu ambayo Wadau wengi wanaamini ili kuwa ni kali mno kupewa kwani aliucheza mpira, walifanikiwa kutoka droo na Aston Villa wakiwa nyumbani Villa Park.
Villa ndio walitangulia kwa bao la kichwa la Carlos Cuellar dakika ya 18.
Man United walisawazisha dakika 3 baadae baada ya krosi ya Nani kumkuta Giggs aliefumua shuti lililombabatiza James Collins na kutinga.
Vikosi:
Aston Villa: Friedel, Cuellar, Collins, Dunne, Luke Young, Petrov, Ashley Young, Milner, Delph, Downing, Agbonlahor.
Akiba: Guzan, Sidwell, Carew, Delfouneso, Davies, Salifou, Beye.
Man United: Van der Sar, Rafael Da Silva, Brown, Jonathan Evans, Evra, Scholes, Carrick, Fletcher, Nani, Rooney, Giggs.
Akiba: Foster, Neville, Owen, Berbatov, Park, Valencia, Gibson.
Refa: Peter Walton

1 comment:

Anonymous said...

LEO BLOG YETU NAONA HABARI KWA UFUPI TU :-)))

Powered By Blogger