Wednesday 10 February 2010

LIGI KUU: Kivumbi leo!!!
RATIBA: Jumatano, Februari 10
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v Liverpool
Aston Villa v Man Utd
Blackburn v Hull
West Ham v Birmingham
Wolverhampton v Tottenham
[saa 5 usiku]
Everton v Chelsea
TATHMINI: Baadhi ya Mechi
Aston Villa v Manchester United
Mechi ipo Villa Park, nyumbani kwa Aston Villa, na Aston Villa watataka waifunge kwa mara ya pili Manchester United kwani katika mechi ya kwanza huko Old Trafford walishinda bao 1-0.
Lakini Man United watataka kusawazisha rekodi yao kwa Villa kwani ushindi huo wa Villa ulikuwa ni wa kwanza katika mechi 25 kati yao.
Katika mechi hii huenda Villa wakamkosa Mshambuliaji Emile Heskey ambae alitolewa katika mechi ya Jumamosi na Tottenham huku akichechemea baada ya kuumia mguu.
Man United watamkosa Rio Ferdinand ambae anatumikia kifungo cha mechi 4 na hii ni mechi yake ya 3 kuikosa.
Vikosi vitatokana na:
Aston Villa: Friedel, Guzan, Beye, Cuellar, Collins, Dunne, L Young, A Young, Petrov, Milner, Downing, Delph, Agbonlahor, Carew, Heskey, Delfouneso, Sidwell, Davies, Clark.
Man United: Van der Sar, Kuszczak, Neville, Brown, Rafael, De Laet, Vidic, Evans, Evra, Fabio, Park, Nani, Valencia, Carrick, Scholes, Fletcher, Gibson, Anderson, Giggs, Rooney, Owen, Berbatov, Diouf.
Refa : Peter Walton
Arsenal v Liverpool
Mechi hii ipo Emirates Stadium ambako katika mechi yao ya mwisho hapo nyumbani Arsenal walitandikwa 3-1 na Manchester United na mechi iliyofuata, siku ya Jumapili, Arsenal walifungwa 2-0 na Chelsea.
Wenyewe Arsenal washatamka mechi hii ni lazima washinde ingawa ni kivumbi kwa vile Liverpool kwa sasa imefufuka na ipo kwenye wimbi la ushindi.
Liverpool watamkosa Difenda wao Sotirios Kyrgiakos anaetumikia kifungo cha mechi 3 baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu walipocheza na Everton.
Vikosi vitatokana na:
Arsenal: Almunia, Sagna, Vermaelen, Gallas, Clichy, Arshavin, Fabregas, Walcott, Song, Nasri, Diaby, Fabianski, Campbell, Denilson, Fabianski, Ramsey, Eboue, Bendtner, Rosicky, Eastmond.
Liverpool: Reina, Skrtel, Agger, Carragher, Insua, Gerrard, Lucas, Rodriguez, Riera, Ngog, Kuyt, Cavalieri, Pacheco, Spearing, Darby, Babel, Aurelio, Degen.
Refa : Howard Webb
Everton v Chelsea
Vinara wa Ligi, Chelsea, leo wapo Goodison Park wakiwa wageni wa Everton huku wakiomba wapinzani wao Man United na Arsenal wakwame katika mechi zao na wao waishinde Everton na kuongeza gepu kwenye pointi.
Everton itamkosa Winga wao machachari kutoka Afrika Kusini Steven Pienaar aliepewa Kadi Nyekundu mechi ya Jumamosi walipocheza na Liverpool.
Pia, Everton itamkosa Kiungo Marouane Fellaini alieumia enka siku na Liverpool.
Chelsea nao watawakosa majeruhi wao wa muda sasa kina Michael Essien, Juliano Belletti na Jose Bosingwa.
Katika mechi ya kwanza huko Stamford Bridge, Timu hizi zilitoka sare 3-3.
Vikosi vitatokana na:
Everton: Howard, Neville, Heitinga, Distin, Baines, Senderos, Yobo, Cahill, Rodwell, Arteta, Osman, Bilyaletdinov, Coleman, Saha, Donovan, Yakubu, Anichebe, Vaughan, Duffy, Baxter, Nash.
Chelsea: Cech, Hilario, Turnbull, Ivanovic, Carvalho, Terry, A Cole, Ballack, Deco, Lampard, J Cole, Malouda, Anelka, Sturridge, Borini, Ferreira, Alex, Zhirkov, Kakuta, Obi.
Refa : Alan Wiley

No comments:

Powered By Blogger