Saturday 13 February 2010

FIFA huenda ikabadili baadhi ya sheria!
FIFA imetoa mapendekezo kwa Bodi ya Soka ya Kimataifa [IFAB] ili kuondoa adhabu tatu kwa mpigo ambazo hutolewa kwa Mchezaji anaemchezea Mchezaji mwingine rafu ndani ya boksi na Refa kuamua Mchezaji huyo aliechezewa rafu alikuwa waziwazi akienda kufunga na hivyo kulazimika kutoa Penalti, Kadi Nyekundu kwa mkosaji na pia baadae mkosaji huyo kufungiwa mechi 3.
FIFA imeona adhabu hizo 3 kwa mpigo ni kubwa mno na hivyo inataka penalti ikitolewa Mchezaji huyo mkosaji apewe Kadi ya Njano tu.
IFAB itakutana Machi 6 kutoa uamuzi
Dondoo nyingine kwenye mkutano huo ni kupiga marufuku Wachezaji wanaopiga penalti kugushi wakati wakikimbia kwenda kupiga mpira kwani sheria ya sasa haikatazi hilo ingawa Refa ana uhuru wa kutoa uamuzi akiona Mpigaji anatenda kinyume cha uanamichezo.
Vingine vitakavyo kuwa kwenye meza ya mjadala ni teknolojia ya kuamua kama mpira umevuka mstari wa golini, na hivyo ni goli au la, na majaribio ya kuwa na Marefa wawili wa ziada wanaokaa nyuma ya kila goli yaliyokuwa yakifanywa kwenye Mashindano ya EUROPA LIGI.

No comments:

Powered By Blogger