Ufaransa Mwenyeji EURO 2016
Ufaransa leo imechaguliwa kuwa Mwenyeji wa Fainali za Mashindano ya EURO 2016 Michuano inayoshirikisha Mataifa ya Ulaya itakayokuwa na Nchi 24 na kuchezwa jumla ya Mechi 51.
Ufaransa iliibwaga Uturuki kwa kura moja na Italia ilitupwa nje katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo.
Kampeni za Ufaransa za kuwania nafasi hiyo ziliongozwa na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Staa wa zamani Zinedine Zidane huko Makao Makuu ya UEFA Nchini Uswisi.
Serikali ya Ufaransa imesema itatoa dhamana ya Pauni Bilioni 1.45 ili zitumike kujenga na kukarabati Viwanja mbalimbali kwa ajili ya Michuano hiyo.
Katika maombi yao ya kuwa Wenyeji Ufaransa ilipendekeza Viwanja 12 ukiwemo ule uitwao Stade de France ambako Ufaransa waliifunga Brazil Mwaka 1998 na kutwaa Kombe la Dunia.
Vingine ni Uwanja wa Klabu ya Paris Saint Germain uitwao Parc des Princes, Lens, Lille, Bordeaux, Nice, Toulouse, Marseille, Lyon, Strasbourg, Saint Etienne na Nancy.
Kabla ya Fainali hizo za EURO 2016, zitafanyika Fainali za EURO 2012 kwa pamoja Nchini Poland na Ukraine na zitashirikisha Nchi 16.
Familia ya Glazer yasema Man United haiuzwi!!!
Familia ya Kimarekani ya kina Glazer imetoa taarifa rasmi leo iliyotamka Klabu yao Manchester United haiuzwi na wao hawana nia ya kumsikiliza Mtu yeyote mwenye azma ya kutoa ofa ya kuinunua.
Tamko hilo ni la kwanza rasmi toka kwa Wamiliki hao tangu ulipoanza upinzani dhidi yao toka kwa Kikundi kinachojiita ‘Wakombozi Wekundu’ ambacho ni Kikundi cha Watu Matajiri Mashabiki wa Manchester United na Kikundi kingine ni cha Masapota kinachoitwa MUST [Manchester United Supporters Trust] ambacho pia kinataka Familia ya Glazer ing’oke Manchester United.
Vikundi hivyo viwili, Red Knights na MUST, vilisema vitakusanya nguvu zao kwa pamoja ili kushinda vita yao.
Wakati MUST ilikuwa ikikusanya nguvu na kuendesha upinzani kwa Mashabiki kuvaa Rangi za Dhahabu na Kijani katika mechi za Man United ambazo ndizo zilikuwa Rangi za Klabu anzilishi ya Man United iliyoitwa Newton Heath, ‘Wakombozi Wekundu’ walikuwa wakikusanya nguvu ya kifedha ili kutoa ofa kwa kina Glazer.
Taarifa hiyo ya Familia ya Glazer imesema Klabu inaendeshwa vizuri na inazalisha fedha nyingi licha ya kuwa na deni kubwa ambalo hata hivyo linalipwa kama ilivopangwa na halisumbui uendeshaji.
Vilevile, taarifa hiyo ilidokeza jinsi Wadhamini wapya, wanaolipa pesa nyingi, wanavyozidi kumiminika na kuwa Timu inategemewa kufanya ziara yenye faida kubwa kifedha huko Marekani na Canada katika Majira ya Joto kabla Msimu mpya wa 2010/11 kuanza hapo Agosti 8.
No comments:
Post a Comment