Baadhi ya mechi za Ligi Kuu zaahirishwa!!
• Wenger ataka mechi zote zisichezwe!!!Hali ya hewa ya baridi kali na barafu mtindo mmoja zimesababisha mechi kadhaa za Ligi Kuu England za hapo kesho ziahirishwe hasa kwa sababu ya usalama wa Washabiki ikizingatiwa barabara kuwa za hatari kwa ajili ya barafu.
Mpaka saa Mechi ambazo hazitachezwa kesho ni:-Fulham v Portsmouth
-Burnley v Stoke
-Sunderland v BoltonMechi kati ya Liverpool v Tottenham ipo kwenye hatihati kubwa hasa baada ya Liverpool kuitaka Ligi Kuu kuiahirisha kutokana na hali ya hewa.
Wakati huo huo, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameitaka LigI kuu kuahirisha mechi zote za Ligi Kuu za wikiendi hii ili kuwe na usawa kwa Timu zote na amedai kuwa ikiwa baadhi tu ya mechi hazitachezwa baadhi ya Timu zitanufaika kwa mechi hizo kuchezwa baadae kwa vile watakuwa washajijua wako nafasi gani katika msimamo wa Ligi.
Pichani juu ni mitutu ya Arsenal nje ya Uwanja wa Emirates ilivyoganda barafu.
Viera ni rasmi Man CityManchester City wamekamilisha usajili wa mkopo wa Patrick Viera kutoka Inter Milan na atakuwa hapo awali kwa miezi 6 na kuna kipengele cha kuongezewa miezi 12 mingine hapo baadae.
Viera, miaka 33, ni Mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Meneja mpya wa Man City Roberto Mancini na wawili hao wanajumuika tena baada ya kuwa pamoja Inter Milan ambako walitwaa Ubingwa wa Italia wa Serie a mwaka 2007 na 2008.
Viera amekuwa akitaka kuihama Inter Milan ambako hakuwa akipata namba ili afanikishe kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni.
Viera ameshachezea Ligi Kuu England alipokuwa Nahodha wa Arsenal na kuihama mwaka 2005 kwenda Juventus alikokaa msimu mmoja tu na kisha kuhamia Inter milan
Gary Neville hastaafu!!
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amepuuza taarifa za Magazeti kuwa Nahodha wake Gary Neville atastaafu soka Msimu huu ukimalizika.
Taarifa hizo zimezagaa hasa baada ya Maveterani wenzake Ryan Giggs na Paul Scholes kuongezewa Mikataba na yeye Neville kutopewa kitu.
Neville, miaka 35, amekuwa akiandamwa na kuumia mara kwa mara katika Misimu ya hivi karibuni lakini Ferguson amesisitiza: “Hamna kilichoamuliwa kuhusu Neville. Kwa nini tuamue hatma yake ya baadae wakati hatuhitajiki kufanya hivyo? Hufanyi maamuzi katikati ya Msimu! Huo ni upuuzi mkubwa!!!”
Dossena wa Liverpool ahamia Napoli
Mlinzi wa Liverpool Andrea Dossena, miaka 28, amehamia Klabu ya Italia ya Serie A Napoli kwa Mkataba wa Miaka minne.
Dossena alijunga na Liverpool mwaka 2008 kutoka Udinese ya Italia kwa Pauni Milioni 7 lakini ameichezea Liverpool mechi 30 tu na kufunga bao 2.
Liverpool pia wapo katika hatua za mwisho za mauzo ya Straika Andriy Voronin ambae atajiunga na Dynamo Moscow kwa Pauni Milioni 2.
Voronin alijiunga na Liverpool mwaka 2007 kutoka Bayer Leverkusen lakini Msimu uliokwisha alikuwa akicheza huko Ujerumani kwa mkopo kwenye Timu ya Hertha Berlin.
No comments:
Post a Comment