Bosi waChelsea, Carlo Ancelotti, ana mipango kamambe ya kuwafanya Mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu kwa Msimu wa 2009/10 wawe wanatawala Soka la England.
Ancelotti, miaka 50, amesema: “Ntakuwa hapa kwa muda mrefu na nategemea kushinda Ubingwa mara nyingi. Tuna Kikosi imara kwa mwaka ujao na mingine.”
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Chelsea, Ron Gourlay, amemuunga mkono Ancelotti na kusema: “Tuna Wachezaji 28 wenye umri wa wastani wa miaka 27 na hivyo si Wazee!”Ancelotti ameongeza kuwa lengo lao kwa sasa ni kulitwaa Kombe la FA ambalo watacheza Fainali na Portsmouth Jumamosi Mei 15 Uwanjani Wembley.
Ancelotti pia amedai kuwa atafanya alichokifanya Meneja wa Chelsea wa zamani, Jose Mourinho, kwa kuchukua Ubingwa mara mbili mfululizo pale alipotwaa Taji la Ligi Kuu mwaka 2005 na 2006.
Ingawa Mourinho alichukua Mataji mawili mfululizo hakuwezi kuutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu na pia Kombe la FA katika Msimu mmoja kitu ambacho Ancelotti anaweza kukitimiza Msimu huu ikiwa watasishinda Portsmouth kwenye Fainali.
Wakati Chelsea wanajipongeza kwa Ubingwa, Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amedai wataibuka upya Msimu ujao na kuurudisha nyumbani Ubingwa wao.
Ferguson ametamka: “Ni lazima tutarudi tena Msimu ujao na kutwaa Ubingwa! Hii ni asili na tabia ya Manchester United! Tutalirudisha Taji kwenye sehemo inayostahili, sehemu bora Duniani!”
Hata hivyo, Ferguson aliwapongeza Chelsea na kusema wamestahili kuwa Mabingwa.
Ferguson amesema: “Hii ni Ligi ngumu Duniani! Kwa Carlo, namwambia hongera!”
No comments:
Post a Comment