Berbatov ajiuzulu Bulgaria, kuendelea Man United
Straika wa Manchester United Dimitar Berbatov amepuuza habari kuwa atahama Manchester United kabla Msimu ujao kuanza na badala yake amesema atabaki Klabuni hapo kupigania namba.
Berbartov, miaka 29, pia ametangaza kujiuzulu kuichezea Timu ya Taifa ya Nchi yake Bulgaria, yeye akiwa Nahodha, ambayo haikufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi ujao na ipo Kundi moja na England kwenye Mchujo wa EURO 2012.
Berbatov ametamka: “Siende popote, nipo Man United! Nimefika nilipopataka na hapa ni kileleni!”
Berbatov alijiunga na Man United mwaka 2008 kutoka Tottenham na katika mechi 65 alizocheza amefunga bao 26 lakini amekuwa akipondwa na baadhi ya Washabiki wa Klabu hiyo wakidai si mhangaikaji na anakosa bao nyingi.
Kuna vyanzo vya habari vimedai Berbatov atahamia Bayern Munich au AC Milan au hata kurudi Tottenham.
Lakini mwenyewe amedai: “Man United ni Klabu kubwa kabisa na ntapigana kubaki hadi Mkataba wangu uishe!”
Mkataba wa Berbatov unakwisha mwaka 2012.
Gallas mguu nje Ze Gunners
William Gallas, ambae Mkataba wake unakwisha kabla Msimu ujao kuanza, huenda asipate nyongeza ya Mkataba wake kufuatia kung’ang’ania kuongezwa Mshahara pamoja na nyongeza hiyo ya Mkataba ya mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood, amedai: “Tunataka abaki lakini madai yake ni makubwa mno na sisi hatuwezi kukubali. Ni Mchezaji mzuri lakini hatuna uwezo wa kumlipa zaidi. Akipata Klabu nyingine bora aende alipwe zaidi!”
No comments:
Post a Comment