Ancelotti: "Kutolewa UEFA kumetusaidia!"
Carlo Ancelotti amekubali kuwa kutokucheza UEFA katikati ya wiki kumewasaidia kuifunga Manchester United tofauti na Manchester United waliocheza mechi huko ujerumani siku ya Jumanne na kurudi England kucheza na Chelsea Jumamosi.
Chelsea wao walicheza mechi yao ya mwisho Jumamosi iliyokwisha na kupumzika wiki nzima.
Man United walicheza na Bayern Munich na wakapata pigo la kuumiziwa Mfungaji wao bora Wayne Rooney.
Chelsea sasa ndio wanaoongoza Ligi kwa pointi mbili mbele ya Man United.
Ancelotti amekiri unafuu walioupata kwa kusema: "Pengine tulinufaika kutolewa UEFA! Tulipumzika na kufanya mazoezi vizuri tu!"
Wenger kujadili hatima yake Arsenal
Arsene Wenger ataketi na Maafisa wa Arsenal mwishoni mwa Msimu ili kufikia makubaliano ya yeye kuongeza Mkataba wake au nini kifanyike.
Mkataba wa Wenger unamalizika mwakani lakini mwenyewe amesema yuko tayari kwa majadiliano. Kumekuwa na tetesi za chini kwa chini ambazo hata yeye ashawahi kuzikanusha kuwa Real Madrid wanamwinda ili ambadili Pellegrini.
Wenger alijiunga na Arsenal mwaka 1996 wakati akiwa hana umaarufu wowote lakini katika miaka 14 aliyokuwa hapo amejizolea sifa kubwa kwa kujenga Timu inayocheza Soka Tamu na kuifanya iwe moja ya Vigogo wa Ulaya.
Hata hivyo, sasa ni miaka mitano tangu Arsenal watwae Kombe kwa mara ya mwisho.
Arsenal walibeba FA Cup mwaka 2005 na huo ukawa ndio mwisho.
1 comment:
KUWA NA HESHIMA NA USTAARABU. WENGER ALIPOKUJA ARSENSL ALIKUWA NA UZOEFU WA KUTOSHA NA UMAARUFU PIA.LABDA WEWE ULIKUWA HUMJUWI KWANI TZ NDO KWANZA MLIANZA KUFATILIA LIGI ZA ULAYA, COZ HAMKUWA NA TV MPAKA MIAKA YA 90. KUBUKA ALIKUWA ONACO NA JAPAN KWA MIAKA NDIO AKAJA HAPA UK.ARSENAL SI KAMA TFF WACHUKUWE KOCHA ASOJULIKANA. SEA WEWE ULIKUWA HUMJUWI
Post a Comment