Wednesday 7 April 2010

Breking nyuziii: Rooney ndani ya Kikosi dhidi ya Bayern Munich!!
Habari kutoka Old Trafford ambako lile pambano la kukata na shoka litaanza muda si mrefu kuanzia sasa kati ya Manchester United na Bayern Munich zimethibitisha kuwa Wayne Rooney amepona enka na anaanza mechi hiyo.
Rooney aliumia katika mechi ya kwanza kati ya Timu hizo wiki iliyopita ambayo Bayern walishinda 2-1.
Kikosi kamili cha Man United kitakuwa:
Van der Sar, Evra, Ferdinand, Rooney, Vidic, Carrick, Nani, Rafael, Fletcher, Valencia, Gibson
El-Hadj Diouf kumsalimi Pilato Mei 10
Straika wa Blackburn, El-Hadji Diouf anaetoka Senegal, atafikishwa Mahakamani Mwezi ujao kwa makosa ya kuendesha gari bila leseni wala bima makosa yanayodaiwa kutendeka huko Manchester Septemba 14 mwaka jana.
Diouf alisimamishwa na Polisi wakati akiendesha gari aina ya Porsche Cayenne na atafikishwa Mahakamani Mei 10 Jijini Manchester.

2 comments:

Anonymous said...

MUME AKIFA NA UKIMWI MKE HUPONI. HONGERA KWA USHINDI 3 KWA 2. BORA MNGEMUACHA ROONEY APONE VIZURI

Anonymous said...

Kaka vp blog imepata kwikwi nini? Au kutolewa na kwa MAN U ndiyo hatupati moto moto. Hata matokeo hutaki kuyaweka! Ama kweli hii ni blog ya Manchester na si soka la England kwa ujumla. Badili jina liwe MAN U BLOGSPOT.

Powered By Blogger